LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi Misungwi kulipwa fidia “kupisha shughuli za jeshi”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Serikali imewatoa hofu baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Kirumba, Kijiji cha Kigongo Kata ya Idetemya wilayani Misungwi ambao maeneo yao yatachukuliwa na Jeshi la Wananchi (JWT) kwa kubainisha kwamba watalipwa fidia.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein ameyasema hayo Januari 21, 2020 baada ya kutembelea eneo linalotarajiwa kuchukuliwa na JWT kwa ajili ya masuala ya kiusalama na kubainisha kwamba Wizara itatuma wataalamu watakaoshirikiana na Halmashauri ili ifikapo mwezi Aprili mwaka huu 2020 zoezi la tathmini liwe limekamilika.

Aidha Waziri Mwinyi amesema eneo linalotarajiwa kuchukuliwa na jeshi ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha usalama wa wananchi katika eneo la Ziwa Victoria pamoja na ujenzi wa mradi mkubwa wa daraja la Kigongo-Busisi ambalo maandalizi tayari yameanza.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ametumia fursa hiyo kuhimiza zoezi la tathmini kufanyika kwa wakati ili wananchi walipwe fidia na kuachia eneo hilo kwani wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu. Nao wananchi wamepongeza hatua hiyo ya Serikali.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein, viongozi na watendaji mbalimbali wakifuatilia ramani ya eneo linalotarajiwa kutumiwa na jeshi la wananchi kwa ajili ya shughuli za kiusalama katika Kitongoji cha Kirumba wilayani Misungwi.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein akizungumza na wakazi wa Kirumba wilayani Misungwi (hawako pichani). Katikati ni Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella na kushoto ni Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akitoa salamu zake kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kigongo wilayani Misungwi wakifuatilia mkutano huo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.