Balozi Kairuki aanika fursa za kibiashara nchini China 'safari imeiva'
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Balozi wa
Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki (pichani) ameeleza fursa lukuki za kibiashara
katika sekta ya madini zilizopo nchini humo na kuwahimiza watanzania
kuzichangamkia kwani ubalozi wao utawasaidia kila hatua.
Balozi
Kairuki alibainisha fursa hizo Januari 24, 2020 jijini Mwanza wakati
akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa madini Tanzania uliolenga kujadili fursa
za uwekezaji, teknolojia, mitaji na masoko ya madini huku akiwasihi wafanyabiashara
wa madini Tanzania kujiandaa na safari ya kutembelea China mwezi ujao ili
kusaka fursa mbalimbali katika sekta ya madini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Maafisa Madini kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifuatilia mkutano huo.
Wadau wa madini wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi meza kuu.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: