LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watanzania wakumbushwa umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, BMG
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika Msaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amezindua kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoa wa Mwanza huku akiwahimiza watanzania kujiunga na bima hiyo kwani licha ya kuimarisha afya pia inaimarisha uchumi.

Akizungumza jana wakati akizindua kampeni hiyo jijini Mwanza, Mwenyekiti huyo wa Bodi ya NHIF Makinda alisema hospitali zipo ila wanashindwa kwenda kutibiwa kwa vile hawana bima kwani Tanzania mpya ni pamoja na wananchi wake kuwa na bima na duniani pote bima ni lazima.

"Ukiugua unatibiwa haraka na unakuwa na uhakika wa kupata matibabu,mambo ya kuugua hayachagui muda na hayana tarehe wakati mwingine unaugua una ela,bima itakua na mtindo na utaratibu wa maisha yako na kufanyakazi kwa uhakika,siyo tu itakuimarisha kiafya bali na kiuchumi na kufanyakazi kwa bidii, kampeni hii siyo ya kisiasa, ni lazima, hivyo wito wangu ni kwamba watanzania mtafute bima ya afya" alisema Makinda.

Pia aliwagiza watumishi wa Mfuko huo kupita nyumba kwa nyumba,mtaani na sehemu za biashara kuelimisha watu kuhusu bima ili watambue umuhimu wa kujiunga na vifurushi hivyo huku watoa huduma za afya ngazi zote kuwa na ubinadamu kwa wagonjwa wakati wakuwapatia huduma za matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alisema, asilimia 34 ya watanzania ndio wapo katika mfumo wa bima ya afya, lengo la mfuko huo ni kuongeza idadi ya wananchi wanaopata huduma ya matibabu kupitia mfumo huo hivyo wamejikita katika kutoa taarifa na hamasa ili wanachama wapate huduma iliyo bora za matibabu na zenye unafuu na zinazopatikana kwa haraka kupitia vituo hivyo vilivyosajiliwa na mfuko huo .

"Mfuko pia umeweka utaratibu mzuri kwa makundi kama bodaboda, waandishi wa habari na machinga ambao kwa umoja wao watajiunga na bima ya afya na kujihakikishia upatikanaji wa matibabu wakati wote,pia ongezeko hili la wananchama linakwenda sambamba na usajili wa vituo vya kutolea huduma kwa kusajilizaidi ya vituo 7000 nchi nzima ili mwanachama apate huduma mahali popote anapokuwa" alisemaKonga.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Mwanza ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dkt.Severine Lalika na baadhi ya viongozi wa dini akiwemo Mratibu Kamati ya Amani Mkoa wa Mwanza Askofu Zenobius Isaya na Sheikh Mkuu wa Mwanza Hassan Kabeke waliwahimiza wakazi wa mkoa huo kujiunga na mpango huo wa vifurushi ili kupata huduma bora za matibabu na zenye unafuu, hivyo wananchi wachangamkie fursa hiyo pamoja nakuona namna gani ya kuzingatia maboresho hayo yanayotolewa na Serikali.

Walisema Serikali inatumia gharama kubwa kuhakikisha taifa linakuwa na watu wenye afya watakaoshiriki katika harakati zote za kuijenga nchi kufikia kwenye uchumi wa viwanda na wa kati , hakuna taifa litafanya shughuli za maendeleo ikiwa wananchi wake afya zao ni dhaifu hivyo hakuna jambo lililo kubwa kama afya.

"Tuna wajibu wa kushiriki hili,hivyo sisi tukiwa kama viongozi wa dini tutatumia nyumba za ibada kuelimisha waumini umuhimu wakujiunga na vifurushi hivi vya bima ya afya cha kuzingatia viongozi wa NHIF lazima wasimame na viongozi wa dini" walisema viongozi hao .

Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Machinga Mkoa wa Mwanza na Mwenyekiti wa Waendesha Bodaboda Mwanza Gerald Nyerembe waliishukuru Serikali kwa kuokoa maisha ya wajasiriamali kwa kutambua vikundi vyao na kuwaona ni watu wenye uhitaji , wataitumia fursa hiyo vyema pamoja na kufanya kazi zao bila tatizo wakiwa na uhakika wa kupata matibabu bila ya usumbufu.

"Tunajua umuhimu wa bima nasi tunaitaji kuwa na afya njema kuna wakati hamna pesa na unaumwa kama unayo bima mkononi utakwenda hospitali bila kuwaza lolote lakini tunaombi hii bima ya vikundi inamtambua mtu mmoja sisi bodaboda tunao wake zetu tunaomba nao waongezwe" alisema Nyerembe.

No comments:

Powered by Blogger.