LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bingwa shindano la Jiachie na Kili Canvas 2020 apatikana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli(kulia) akimkabizi, Athuman Hamis hundi ya Shilingi milioni mbili(2,000 000/=) mara baada ya kuibuka bingwa kwenye shindano la Sanaa ya Uchoraji lililofanyika jana katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.Athumani pamoja na ushindi huo atapata nafasi ya kuchora Cavas kubwa(Karatasi ngumu) itakayotumika katika sehemu tofauti kuelekea kilele cha Kilimanjaro Marathoni.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli(kulia) akimkabizi, Athuman Hamis pesa taslimu shilingi laki mbili kama pongezi pamoja na hundi ya Shilingi milioni mbili(2,000 000/=) mara baada ya kuibuka bingwa kwenye shindano la Sanaa ya Uchoraji lililofanyika jana katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.Athumani pamoja na ushindi huo atapata nafasi ya kuchora Cavas kubwa(Karatasi ngumu) itakayotumika katika sehemu tofauti kuelekea kilele cha Kilimanjaro Marathoni.
Bingwa wa shindano la Sanaa ya Uchoraji, Athuman Hamis akielezea picha yake aliyomfanya kuingia tano bora na kupata nafasi ya kuchora Mubashara na mwisho kutwaa ubingwa wa shindano hilo lililofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam jana.
Bingwa wa shindano la Sanaa ya Uchoraji, Athuman Hamis akianza kuchora mubashara mara baada ya kuingia tano bora.
Bingwa wa shindano la Sanaa ya Uchoraji, Athuman Hamis akimaliziaa kuchora mubashara mara baada ya kuingia tano bora.

Msanii wa Sanaa kuchora Athuman Hamis kutoka Mwenge Vinyango jijini Dar es Salaam ameibuka kuwa bingwa katika shindano la Sanaa ya Uchoraji lililo fanyika jana katika Hoteli ya Golden Tulipo kwa udhamini wa Kampuni ya Bia Nchini(Tbl) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro kuelekea kilele cha mbio za Kilimanjaro Marathoni 2020, ijulikanalo kama “Jiachie na Kili Canvas competitions 2020”.

Athuman alitwaa ubingwa huo kutoka katika jumla ya Wasanii kumi na tisa(19) waliojitokeza kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania ambapo kwa hatua ya kwanza aliingia tano bora na wote watano kupaswa kuonyesha umahili wao kwa kuchora mbashara mbele ya Majaji na mwisho Athuman Hamis alifanikiwa kuwa bingwa katika shindano hilo.

Athuman kwa ushindi huo alipewa nafasi ya kuchora Canvas kubwa na Kampuni ya Bia Nchini kupitia Bia yake ya Kilimanjaro itakayotumika katika sehemu tofauti kuelekea kilele cha mbio za Kilimanjaro Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Machi 1,2020 Mkoani Kilimanjaro pamoja na pesa taslimu shilingi milioni mbili(2,000 000/=).

Mshindi wa pili mpaka wa tano walizawadiwa pesa taslimu Shilingi laki mbili kila mmoja(200,000/=) ambao ni Donath Kabonda kutoka Chuo Kikuu cha Kampala Gongo la Mboto, Moses Martin kutoka Mwenge Vinyago, August Tairo kutoka Kijitonyama na George Nyandiche kutoka Morogoro Store Osterbay.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, alisema kuwa mashindano haya yalishirikisha Wasanii wa uchoraji wa Nchi nzima. Msanii alitakiwa kuja na kazi aliyoichora kwenye Canvas(kitambaa kigumu cha kuchorea) ikihausianisha bia ya Kilimanjaro, Mlima Kilimanjaro, Nyota tano na mnyama Twiga.

Kikuli alisema, mashindano hayo yalifanyika kwajili ya kutoa fursa kwa Wasanii wa Sanaa ya uchoraji ili waonyeshe kazi zao kwa jamii, kuibua vipaji vipya pamoja na kuongeza mwamko wa tasnia ya Sanaa ya uchoraji Nchini.

Mwisho Kikuli aliwapongeza washindi wote walioingia tano bora lakini zaidi alimpongeza Bingwa Athumani Hamis kwa ushindi na kumuomba ajiandae vyema sasa kuchora mchora ambao utatumika katika maeneo tofauti kwa kuwakilisha pia Sanaa ya ucharaji kwa Watanzania wote.

Pesa uliyopewa kama Zawadi ikawe chachu ya kufanya vizuri na kujiendeleza katika tasnia yako ya Uchoraji.

Nae Jaji Mkuu wa Mashindano ya “Jiachie na Kili Canvas Competition”, Nathan Mpangala alisema mchakato wa kumpata bingwa ulikuwa mgumu sana pamoja na kwamba wasanii walikuwa na muda mchache sana wa kujianda.

Wasanii waliojitokeza kila mmoja alikuwa amejiandaa vikali kuonyesha umahili katika tasnia yake ya uchoraji anaionyesha aknifu kwa kuonyesha kwa vitendo nini alipaswa kufanya lakini pamoja na mchakato wote huo mwisho umetupa bingwa ambaye kila mmoja ameridhia kuwa anastahili kwa namna alivyoonyesha taaluma yake mubashara katika hatua na mwisho.

Nathan aliwapongeza Wasanii wote waliojitokeza kushiriki shindano hilo kwa mwaka 2020 na kuwaomba wajitokeze kwa wingi wakisikia tena kuna fursa kama hiyo si ya kuacha.

No comments:

Powered by Blogger.