LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko kuongoza mkutano mkubwa wa wadau wa Madini jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko Ijumaa Januari 24, 2020 anatarajiwa kuongoza mkutano mkubwa wa wadau wa madini Tanzania utakaojikita kujadili fursa za uwekezaji, teknolojia, mahitaji pamoja na masoko ya madini.

Mkutano huo umepangwa kufanyika katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza ukihudhuria pia na viongozi mbalimbali akiwemo Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki, Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke, Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella pamoja na Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) John Bina.

No comments:

Powered by Blogger.