LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Magufuli aisafisha Wizara ya Mambo ya Ndani "wengine watakiwa kujitathimini"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa uzinduzi wa nyumba za askari magereza katika eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii
AMEONDOLEWA! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Rais Dk.John Magufuli kutangaza kumuondoa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola kutokana tuhuma za kusainiwa kwa mkata wa hovyo ambao baadhi ya maofisa wa Wizara hiyo wameusaini.

Mbali ya Lugola kutakiwa na Rais kuachia nafasi hiyo, pia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni tayari ameshajiuzulu na hata kwenye uzinduzi wa nyumba mpya za askari magereza zilizopo Ukonga jijini Dar es Salaam hakufika. Pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani naye ameshajiulu.

Rais Magufuli katika kuonesha kusikitishwa na miradi ya hovyo ndani ya Wizara hiyo ukiwemo huo wa zaidi ya Sh.trilioni moja ambao umeingiwa na baadhi ya maofisa wa Wizara hiyo, Kamishna Jenereli wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye naye ametakiwa kuachia ngazi nafasi yake hiyo huku pia maofisa kadhaa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu nao wakitakiwa kujitathimini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa nyumba za askari magereza katika eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam , Rais Magufuli pamoja na kupongeza ujenzi wa nyumba hizo, ametumia nafasi hiyo kuelezea kusikitishwa na yanayoendelea katika Wizara ya Mambo ya Ndani.

"Kama kuna Wizara inanitesa basi ni Wizara ya Mambo ya Ndani, nataka muelewe hivyo Watanzania, inanitesa sana. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia kuna tume nyingi zimeundwa kwa ajili ya kuchunguza mamiradi ya hivyo.

"Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani hayupo hapa leo hii, tayari amejiuzulu.Kuna mradi wa hovyo umeingiwa na Wizara hiyo ambao fedha zake ni zaidi ya Sh.Trilioni 1.3.Mradi huo umesainiwa na kuudhinishwa na Kamishna wa Zimamoto na Uokoaji Faya, haujapangwa na Serikali na wala haujaidhinishwa na Bunge.

"Watu waliokuwa wanakwenda kwenye vikao kwa ajili ya kujadili mradi huo walikuwa wanalipwa mamilioni ya fedha.Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani.

amewajibika kwa kuandika barua ya kujiuzulu, nampongeza kwani hata kama hakufanya yeye lakini ni jambo ambalo lipo kwenye wizara yake.Nitaendelea kumheshimu kwa uamuzi wake huu,"amesema Rais Magufuli.

Wakati Rais anaelezea kuhusu mradi huo ambao ameuita ni wa hovyo, amemwambia Lugola kuwa anampenda sana na ni mwanafunzi wake lakini kwenye hilo hapana."Andengenye umefanya kazi nzuri, umejenga nyumba hizi, umeenda hadi Chato lakini kwa hili hapana! ,umeenda mpaka Ulaya na kuchukua fedha kwa ajili ya mradi huo".

Rais Magufuli alipokuwa akiendelea kuzungmza amesema kwanza ameshangaa kuendelea kumuona Lugola akiwa katika shughuli hiyo ya uzinduzi wa nyuma za askari magereza."Anayetaka kufanya kazi na mimi nataka yafanye yale ninayotaka , kama hawezi aende.

"Katika uwatala wangu sitavumilia mambo ya hovyo hovyo, kama wanataka kufanya mambo ya hovyo wasubiri nikiondoka madarakani , wakati huo niko Chato ili huyo ambaye atakuwa anavumilia waendelee naye, sio mimi,"amesema Rais Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa anafurahiswa sana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa kwani kila kazi ambayo wanapewa wanaifanya vizuri na kwa wakati sahihi.

No comments:

Powered by Blogger.