LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mtendaji Mkuu BRELA aanza kazi rasmi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Robertha Makinda - BRELA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa Januari 23, 2020 amewasili rasmi katika kituo chake kipya cha kazi BRELA Ofisi Kuu Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili, Nyaisa amepata wasaa kukaa kikao kifupi na Menejimenti, kutambulishwa kwa wafanyakazi pia kukutana na baadhi ya wadau wa BRELA waliokua wakipata huduma kwa siku ya leo.

Katika maneno yake ya utambulisho kwa wafanyakazi wa BRELA amewataka wampe ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii.

“Wafanyakazi wanzangu naomba kwa kipindi hiki tushirikiane ili tuweze kufanya kazi za serikali ni matumaini yangu kila mmoja atasimama katika nafasi yake na kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha azma ya Tanzania ya Viwanda na kuwa nchi ya uchumi wa kati”, alisema Nyaisa.

Aidha alipokua akizungumza na wadau wa BRELA waliokuwa wakipata huduma siku ya leo, amewaomba waweze kuwa wavumilivu kwa kwa kipindi hiki wakati BRELA inajipanga kutoa huduma bora na kuondoa malalamiko yaliyopo, alibainisha Nyaisa.

Nyaisa aliteuliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA tarehe 19 Januari, 2020 akichukua nafasi ya Loy Muhando aliekuwa akikaimu nafasi hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa (Mwenye tai nyekundu) akisalimiana wadau wa BRELA alipokua akitembelea Ofisi za Idara na Vitengo mbalimbali baada ya kuwasili Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa (Mwenye tai nyekundu) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Leseni BRELA Andrew Mkapa mara baada ya kuwasili Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji Bakari Mketo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa akifafanua jambo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa (mbele) Akizungumza na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo Mbalimbali BRELA mara baada ya kuwasili Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

No comments:

Powered by Blogger.