LIVE STREAM ADS

Header Ads

TANESCO Mkoa Mwanza wasogeza huduma karibu na wananchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa Mwanza limesogeza huduma zake karibu na wananchi kwa kuwafuata katika mitaa yao ili kuwaelimisha kuhusu matumizi sahihi ya nishati ya umeme pamoja na kusikiliza kero zao kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.

Akizungumza Januari 31, 2020 katika Mtaa wa Mirongo jijini Mwanza, Afisa Mahusiano Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa Mwanza, Flaviana Moshi amesema hatua hiyo itawaondolea wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Wananchi katika Mtaa wa Mirongo jijini Mwanza wakipata elimu kuhusu nishati ya umeme katika banda la TANESCO.
 Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakitoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma ya nishati ya umeme, kupokea maoni, kero na malalamiko kwa ajili ya kuboresha zaidi huduma za shirika hilo.
 Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa Mwanza wakimhudumia mteja aliyefika kwenye banda la shirika hilo katika Mtaa wa Mirongo.
 Wananchi jijini Mwanza wakiwa kwenye banda la TANESCO kupata elimu kuhusu nishati ya umeme, kutoa malalamiko na maoni kuhusu huduma za nishati ya umeme.
 Wananchi jijini Mwanza wakipata elimu kuhusu nishati ya umeme hususani kifaa cha UMETA ambacho kinarahisisha huduma ya mteja kuunganishiwa umeme.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO Mkoa mwanza wakiwa wameshika kifaa cha UMETA kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.