Viongozi UWT watakiwa kuacha ubinafsi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Viongozi wa Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT) wametakiwa kuacha ubinafsi na badala yake wazidi
kushirikiana na wanachama wa umoja huo ili kufanikisha ushindi wa CCM katika
Uchaguzi Mkuu 2020.
Rai hiyo ulitolewa Januari
04, 2019 na mmoja wa waasisi wa UWT nchini, Balozi Getrude Mongella wakati
akizungumza kwenye kikao cha Kamati Tendaji ya umoja huo ngazi ya Mkoa Mwanza.
Kauli hiyo iliungwa
mkono pia na Mwenyekiti wa UWT Mkoa Mwanza, Hellen Bogohe aliyesema ubinafsi
miongoni mwa baadhi ya viongozi wa UWT umekuwa kikwazo kwa wanawake kuchaguliwa
kwenye nafasi mbalimbali za uongozi.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: