LIVE STREAM ADS

Header Ads

Zaidi ya milioni 30 kujenga vyoo Tarime

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Mhe Esther N. Matiko ameamua kuokoa Jahazi katika Shule za Sekondari na Msingi kwa kujenga Vyoo vya Wanafunzi na Walimu kwa mwaka wa Masomo ulioanza 06/01/2020.


Kutokana na idadi kubwa ya Wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha Kwanza 2020, kumesababisha idadi kubwa ya wanafunzi waliofaulu kukosa Shule za kujiunga ili kuendelea na Masomo yao ya Sekondari. Jimbo la Tarime Mjini ni Jimbo lilofanikiwa kuanzisha Shule mpya tatu (3) za Sekondari ambazo ni Nkongole, Tagota na Sabasaba ili kutoa nafasi kwa Wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza.



Moja ya Changamoto kubwa inayozikabili Shule hizo ili zianze kutoa Masomo kwa Wanafunzi ni Miundombinu ya Vyoo kwa Wanafunzi na Walimu maana Shule hizo ni mpya ambazo zinajengwa kwa nguvu za Wananchi na Wadau wengine wa Elimu akiwemo Mhe Esther N. Matiko.



Ili kuhakikisha Shule hizo zinaanza kutumika mara moja Mhe Matiko ameamua kujenga Vyoo vya Shule mbili za Sekondari (Tagota na Sabasaba) na Shule moja ya Msingi (Buhemba) iliyokuwa ifungwe baada ya kukosekana kwa Choo, Choo hizo zitajengwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Jimbo Tsh 33,000,000/= mwaka wa fedha 2019/2020.

Shule ya Sekondari Sabasaba tayari imekwishaanza ujenzi wa Matundu 10 ya Vyoo baada ya kupatiwa Millioni Kumi na Mbili na Laki Tano ( Tsh 12,500,000/=) na Mhe Matiko kutoka fedha za Mfuko wa Jimbo. Shule ya Sekondari Sabasaba inabeba wanafunzi waliofaulu kutoka Shule za Msingi za Azimio, Mapinduzi na Sabasaba.


Itakumbukwa katika ujenzi wa Madarasa 7 yaliyojengwa Shuleni hapo Mhe Matiko amepata kuchangia Mifuko 20 ya Saruji kwa fedha zake mwenyewe na Mifuko 50 ya Saruji kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo 2017/2018 na Bati 120 zilizotumika kueezeka Madarasa mawili ya Shule hiyo.



Shule ya Sekondari Tagota ni miongoni mwa Shule zilizonufaika na mgawanyo wa fedha hizo kwa ajili ya Ujenzi wa Matundu 10 ya Vyoo kwa Wanafunzi na Walimu ambapo ujenzi huo tayari umeshaanza. Mhe Esther Matiko ameipatia Shule ya Sekondari Tagota Millioni Kumi na Mbili na Laki Tano (Tsh 12,500,00/=) kama ilivyokuwa kwa Shule ya Sekondari Sabasaba.



Shule ya Sekondari Tagota nayo pia imejengwa kwa nguvu za Wanachi (Mitaa 4 ya Tagota, Kebaga, Kogete na Mwibari) kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Elimu. Katika ujenzi wa Madarasa 4 yaliyojengwa Shuleni hapo Mhe Matiko alichangia Bati 225 zilizotumika kueezeka Madarasa hayo pamoja na Ofisi ya Walimu.

Shule ya Msingi Buhemba ni Shule iliyokumbwa na Zahama ya kutaka kufungwa baada ya Choo kilichokuwa kikitumika kujaa na Wanafunzi kukosa Choo cha kutumia. Wazazi wanaosemesha watoto wao Shuleni hapo waliamua kuaanza ujenzi wa Choo kipya cha Matundu 10 ili watoto wao wasirudi nyumbani.

Mhe Mbunge Esther N. Matiko ameamua kuwapunguzia makali ya michango wazazi hao na kuamua kubeba Mzigo wa ujenzi wa Choo hicho kwa kutoa Millioni Nane (Tsh 8,000,000/=) zitakazotumika kumalizia ujenzi wa Choo hicho cha Matundu 10.

Lakini pia ni vyema ikakumbukwa Katika ujenzi wa Choo hicho Mhe Matiko alipata kuungana na Wananchi awali kwa kuchangia Mifuko 20 ya Saruji kwa fedha zake Mwenyewe na Mifuko hiyo ya Saruji itumika katika ujenzi wa Boma la Choo hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti Walimu, Wazazi na Wanafunzi wamemshukuru sana Mhe Matiko kwa jitihada zake anazozifanya ili kuhakikisha Watoto wa Tarime wanapata elimu na maendeleo mengine kwa ujumla.

Mwl Kivuyo ni Mkuu wa Shule ya Msingi Buhemba alisema, "Mhe Matiko wewe ni wa Mfano wa kuigwa hakika hatutosita kukupa ushirikiano na fedha hizi ulizotupatia amini zitafanya kazi iliyokusudiwa na kama kuna salio litabaki tunakuomba sana tulitumie kuvutia Umeme Shuleni kwetu, zile Computer ulizotupatia zianze kufanya kazi mara moja"

Mhe Esther Matiko alitumia nafasi hiyo kukubali Ombi la Mkuu wa Shule hiyo kuvuta Umeme kwa Salio litakalobaki ukizingatia aliwapatia Computer kwa ajili ya machapisho shuleni hapo ali hali Shule hiyo haikuwa na umeme.

Vile vile Mhe Matiko alitoa Wito kwa wote wanaohusika na Matumizi ya fedha hizo kuhakikisha zinatumika vizuri na kumaliza kazi iliyokusudiwa, lakini pia amewaomba wadau wote wa elimu kujitokeza katika kusaidia Gurudumu la elimu ili liweze kusonga mbele.

Tarime Yetu Mshikamano Kwa Wote
Rasirimali Zetu Kwa Maendeleo Yetu.
Imetolewa na:-
Peter Magwi Michael
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Tarime Mjini.

No comments:

Powered by Blogger.