LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kongamano la CORONA kufanyika jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
KONGAMANO LA ELIMU JUU YA UGONJWA WA CORONA KWA WAANDISHI WA HABARI.

Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC), ni balozi wa mradi wa Boresha Habari chini ya Shirika la Habari la Internews.

MPC imefanya tafiti na kugundua kuwa, kuna hitaji kubwa la waandishi wa habari kufahamu vizuri virusi vya corona, dalili zake na njia za kujikinga ili waweze kuandika habari za uelimishaji kwa jamii juu ya ugonjwa huo, ni wazi kuwa kuna ombwe kubwa katika eneo hilo na uibukaji wa habari zisizo za kweli/fake news.

Kwa kutambua umuhimu huo, MPC imeandaa kongamano la waandishi wa habari Mkoani Mwanza ili kujenga uelewa juu ya virusi vya corona.

Kwa kutambua umuhimu huo MPC kwa kushirikiana na Serikali kupitia ofisi ya Mganga mkuu wa Mwanza itakuwa na kongamano hilo la kujenga uelewa.

Mtoa mada katika kongamano hilo atakuwa, Mganga Mkuu wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa. 

Kongamano hilo litafanyika kesho Februari 24,2020 jijini Mwanza kwenye ukumbi wa Mdogo wa Nyanza, Jijini Mwanza,kuanzia saa 4:00 Asubuhi.

Popote ulipo Mwandishi wa habari na mmiliki wa chombo cha habari unakaribishwa kuhudhuria bila kikosa. 

Limetolewa na;
Kamati Tendaji 
MPC 
23/02/2020

No comments:

Powered by Blogger.