Kufikia Uchumi wa Viwanda "vyuo vyatakiwa kuandaa mitaala inayotoa ujuzi"
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii na Ufundi Tanzania vimetakiwa kuandaa mitaala inayotoa ujuzi
na stadi muhimu zinazohitajika katika soko la ajira ikiwemo viwanda ili
kuwawezesha wahitimu wake kujiajiri na kuajiri watu wengine.
Mkurugenzi
na Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Vickness Mayao aliyasema hayo
Februari 24, 2020 jijini Mwaanza wakati akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu
kwenye kongamano la wadau Kanda ya Ziwa kujadili utekelezaji wa dhana ya
Uanagenzi.
Mayao
alisema Uanagenzi ni dhana inayolenga kuimarisha ujuzi kwa wahitimu hivyo
kongamano hilo lililowahusisha wadau mbalimbali wakiwemo waajiri kutoka taasisi
binafsi na za Serikali litasaidia kupata mikakati ya pamoja ya kutekeleza vyema
dhana hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi na Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Vickness Mayao akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu kwenye kongamano la wadau Kanda ya Ziwa kujadili namna ya kutekeleza dhana ya Uanagenzi.
Viongozi mbalimbali meza kuu akiwemo mgeni rasmi Mkurugenzi na Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Vickness Mayao (katikati) aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu kwenye kongamano la wadau kujadili utekelezaji wa dhana ya Uanagenzi.
Wadau na Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye kongamano la kujadili namna ya kutekeleza dhana ya Uanagenzi.
Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye kongamano hilo.
Wadau mbalimbali waliohudhuria kongamano la kujadili namna ya kutekeleza dhana ya Uanagenzi Kanda ya Ziwa.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: