LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wajasiriamali mkoani Mwanza wanufaika na mafunzo kutoka SIDO

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shirika la kuhudumia miwanda vidogo Tanzania (SIDO) Mkoa Mwanza lietoa mafunzo kuhusu usindikaji wa vyakula na vinywaji kwa wajasiriamali zaidi ya 40 mkoani Mwanza, lengo likiwa ni kuwajengea ujuzi wa kujiajiri na kujipatia kipato.

Mafunzo hayo yalihitimishwa na Februari 07, 2020 na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa Mwanza, Leopord Lema ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Mwanza Quality Wines inayojihusisha na utengenezaji wa mvinyo wa matunda wa Power Banana.

Baada ya mafunzo hayo, wajasiriamali hao walishauriwa kutumia vyema miongozo inayotolewa na SIDO ili kurasimisha biashara zao na kuzingatia taratibu za Serikali ikiwemo kulipa kodi huku changamoto zilizopo kama gharama za vifungashio zikiendelea kushughulikiwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa Mwanza, Leopord Lema akizungumza kwenye kilele cha mafunzo hayo.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa Mwanza, Leopord Lema alitoa rai kwa wajasiriamali kushirikiana vyema na watakaowakuta sokoni ili kujiimarisha zaidi.
Wajasiriamali waliopata mafunzo SIDO wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa Mwanza, Leopord Lema.
Mmoja wa wajasiriamali walionufaika na mafunzo kutoka SIDO alisema moja ya changamoto inayowakumba wajasiriamali ni pamoja na ukosefu wa mitaji.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa Mwanza, Leopord Lema akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa amfunzo hayo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.