MWANZA- Fuatilia ujenzi wa Soko la Kisasa Kiloleli
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Baada ya
kufanya utafiti na kubaini wafanyabiashara wadogo hususani wanawake wanakabiliwa
na mazingira magumu ya kufanyia biashara, shirika la kutetea haki za wanawake
na wasichana (KIVULINI) limesaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uboreshaji
wa soko la Kiloleli lililopo Wilaya Ilemela pamoja na Mirongo katika Wilaya ya
Nyamagana.
Uboreshaji
wa masoko hayo unahusisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu bora na rafiki
kibiashara ikiwemo vyoo, mitaro ya kuzuia maji kuingia sokoni, eneo maalumu kwa
watoto kuchezea na akina mama kunyonyeshea pamoja na Kituo cha daladala
Kiloleli.
Soko la Kiloleli
linatarajiwa kugharimu shilingi Milioni 127 ikiwa ni pamoja na miundombinu
iliyotajwa hapo juu huku soko la Mirongo likigharimu shilingi Milioni 90.8
ambapo ujenzi huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi mitatu
kuanzia mwezi Februari 2020.
Ungana na
BMG TV kutazama hatua ulipofikia ujenzi, ukarabati na uboreshaji wa soko la
Kiloleli.
SOMA PIA>>> Ujenzi soko la Kisasa Mirongo
No comments: