LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maboresho soko la Mirongo jijini Mwanza yaanza “litakuwa la mfano”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella Machi 10, 2020 amekagua maboresho ya soko la wafanyabiashara wadogo Mirongo lililopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kutoa pongezi kwa shirika la KIVULINI amblo limesaidia upatikanaji wa fedha kutoka kwa wadau kwa ajili kuboresha soko hilo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Baada ya kufanya utafiti na kubaini wafanyabiashara wadogo wanakabiliwa na mazingira magumu ya kufanyia shughuli zao, Shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana (KIVULINI) kwa kushirikiana na Shirika la misaada kutoka Uingereza (I4ID) limeanza ujenzi wa masoko ya kisasa mkoani Mwanza yatakayokuwa mfano pia katika kuboresha masoko mengine nchini.
Masokoko hayo yanajengwa katika eneo la Kiloleli Manispaa ya Ilemela pamoja na Mirongo jijini Mwanza yakihusisha miundombinu bora na rafiki kibiashara ikiwemo vyoo, eneo maalumu kwa akina mama kunyonyeshea pamoja na Kituo cha daladala Kiloleli.
Soko la Kiloleli linatarajiwa kugharimu shilingi Milioni 127 huku soko la Mirongo likigharimu shilingi Milioni 90.8 ambapo ujenzi huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Februari 2020.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.