LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mongella akagua miradi ya maendeleo jijini Mwanza "aagiza ikamilike haraka"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella Machi 10, 2020 amekagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kisha kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Igoma kusikiliza kero zao ili kuzitafutia ufumbuzi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua ujenzi wa barabara ya Isamilo-Nyashana inayojengwa kwa kiwango cha mawe.
 Ujenzi wa barabara ya Isamilo-Nyashana jijini Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) akishiriki ujenzi wa barabara ya Isamilo-Nyashana inayojengwa kwa kiwango cha mawe.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella pia alikagua ujenzi wa jengo la wazazi/ wodi ya mama na mtoto katika Zahanati ya Mahina.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizindua wodi ya mama na mtoto katika Zahanati ya Mahina jijini Mwanza.
 Mwonekano wa wodi ya wazazi/ mama na mtoto katika Zahanati ya Mahina.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alikagua pia ujenzi wa vyumba sita vya madarasa katika Shule ya Msingi Mandela iliyopo Kata ya Igoma.
 Mwonekano wa baadhi ya vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Mandela.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba sita vya madarasa katika Shule ya Msingi Mandela Kata ya Igoma na kuagiza ujenzi huo kukamilika ifikapo Aprili Mosi 2020.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akitoa salamu zake kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa Mwanza kuzungumza na waalimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mandela.
 Wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mwanza (hayuko pichani) alipofanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Igoma.
 Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akisalimia wananchi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ili kuzungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Igoma.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza na wananchi kupotia mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Igoma.
 Wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.