LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Nyamagana asaka barakoa kwa ajili ya mahabusu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Mkuu wa Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza, Dkt. Philis Nyimbi amewahmiza wadau mbalimbali kuendelea kusaidia upatikanaji wa vifaa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa ajili ya jeshi la polisi.

Dkt. Nyimbi ameyasema hayo wakati akipokea vifaa vya kujikinga na Corona vilivyotolewa na Shirika la KIVULINI kwa jeshi la polisi mkoani Mwanza na kuongeza kwamba jeshi hilo bado linahitaji vifaa zaidi ikiwemo barakoa ambazo ni muhimu pia kwa mahabusu.

Shirika la KIVULINI limesaidia upatikanaji wa tenki la maji lita 1,000, kifaa cha kupimia joto la mwili pamoja na vitakasa mikono kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya Corona katika Ofisi za Jeshi la Polisi mkoani Mwanza vikiwa na thamani ya shilingi milioni 1.2.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Pia Shirika la KIVULINI limepeleka tenki ya maji lita 1,000, kifaa cha kupimia joto la mwili pamoja na vitakasa mikono katika masoko ya Mirongo na Kiloleli jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.