LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA "wananchi kupimwa joto masokoni"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (kulia) akimpima joto la mwili mmoja wa akina mama katika soko la Mirongo jijini Mwanza baada ya Shirika la KIVULINI kukabidhi vifaa vya kusaidia mapambano dhidi ya maambukizi ya Corona sokoni hapo. 

Vifaa hivyo ni pamoja na tenki la maji lita 1,000, mashine ya kupimia joto la mwili pamoja na vitakasa mikono vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 2.4.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia) akimkabidi Mganga Mkuu Wilaya Ilemela mashine ya kupimia joto la mwili kwa ajili ya kutumika katika soko la Kiloleli wilayani humo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza wakati wa kukabidhi tenki la maji, mashine ya kupimia joto la mwili pamoja na vitakasa mikono katika soko la Kiloleli Manispaa ya Ilemela.
 Wafanyabiashara wakiwemo akina mama katika soko la Kiloleli wakinawa mikono kwa maji tiririka baada ya Shirika la KIVULINI kukabidhi tenki la maji lita 1,000.
Shirika la KIVULINI limesaidia ujenzi wa Soko jipya la Kiloleli Manispaa ya Ilemela kama linavyoonekana pichani.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA SOMA>>> Habari za Corona

No comments:

Powered by Blogger.