LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shehena ya dawa za Serikali yakamatwa Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Mwanza imekamata shehena ya dawa za kilimo zenye thamani ya shilingi milioni 12 (Tsh. 12,609,000) zikiiuzwa kinyume na utaratibu katika maduka ya wafanyabiashara jijini Mwanza.

Mkuu wa TAKUKURU mkoani Mwanza, Emmanuel Stenga amesema dawa hizo zilinunuliwa na Serikali kupitia Bodi ya Pamba kwa ajili ya wakulima katika Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS).

Aidha Stenga amebainisha kwamba TAKUKURU Mkoa Mwanza inamshikiria Mhasibu wa AMCOS ya Mhedi iliyopo Kishapu mkoani Shinyanga, wafanyabiashara 13 pamoja na madalali watatu kwa tuhuma za kuhusika na biashara ya dawa hizo katika maduka mbalimbali jijini Mwanza.
#BMGHabari
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.