LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakazi wa Nyamongo waanza kulipwa fidia ‘waliotegesha hola’

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Wananchi wa Nyamongo wilayani Tarime Mei 20, 2020 wameanza kupokea hundi za malipo ya fidia ya ardhi ili kupisha shughuli za mgodi wa North Mara unaoendeshwa kwa ubia baina ya Serikali na kampuni ya Barick kupitia kampuni tanzu ya Twiga.

Viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula wameshuhudia zoezi la upokeaji hundi hizo ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 30 zinatarajiwa kulipwa kwa wakazi 1,639 wa Nyamongo katika awamu ya kwanza.
#BMGHabari
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kulia) akimkabidhi hundi mmoja wa wanufaika wa fidia ya ardhi katika eneo la Nyamongo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (katikati) akimkabidhi hundi mmoja wa wanufaika wa fidia ya ardhi katika eneo la Nyamongo. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) na kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.