LIVE STREAM ADS

Header Ads

BITEKO achukua maamuzi magumu waliogomea FIDIA Nyamongo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Wakazi wa Nyamongo wilayani Tarime ambao waligomea hundi za fidia kutoka mgodi wa dhahabu North Mara, wametakiwa kuchukua hundi zao ndani ya muda wa wiki mbili uliotolewa na Mkuu wa Mkoa Mara, Adam Malima kwani muda huo ukiisha watakosa haki hiyo.

Waziri wa Madini, Doto Biteko (juu) aliyasema hayo Mei 20, 2020 wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa zoezi la ugawaji hundi kwa wananchi 1,639 wa Vijiji vya Matongo na Nyabichune ili kupisha ardhi yao kwa ajili ya shughuli za mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Barick pamoja na Serikali kupitia kampuni tanzu ya Twiga. 
#BMGHabari
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akitoa salamu zake wakati wa ufunguzi wa zoezi la kukabidhi cheki/ hundi kwa wanakazi wa Nyamongo ambao wanapisha ardhi yao kwa ajili ya shughuli za mgodi wa North Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu akitoa salamu kwa wananchi.
 Mkuu wa Mkoa Mara, Adam Malima akitoa salamu wakati wa zoezi la kukabidhi hundi kwa wakazi wa Nyamongo.
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema benki hiyo imejipanga vyema kutoa elimu ya kifdha pamoja na malipo kwa wananchi wanaopokea hundi za fidia ya ardhi kutoka mgodi wa Nyamongo North Mara.
Wakazi wa Nyamongo wakifuatilia ufunguzi wa zoezi la kukabidhi hundi/ cheki kwa wananchi ambao ardhi yao inachukuliwa na mgodi wa Nyamongo North Mara.  
Wakazi wa Nyamongo wakifuatilia ufunguzi wa zoezi la kukabidhi hundi/ cheki kwa wananchi ambao ardhi yao inachukuliwa na mgodi wa Nyamongo North Mara. 
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiteta jambo baada ya kutembelea shimo la kuhifadhia maji sumu (TFS) katika mgodi wa Nyamongo North Mara. Viongozi wengine ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula pamoja na Mkuu wa Mkoa Mara, Adam Malima.
Eneo la shimo la kuhifadhia maji sumu (TFS) katika mgodi wa Nyamongo North Mara. 
Moja ya shimo lililokuwa likichimbwa madini ya dhahabu (Rama Pit) katika mgodi wa North Mara ambalo kwa sasa linahifadhi maji kutoka kutoka eneo la maji sumu (TFS) ikiwa ni jitihada za kuzuia maji hayo kuingia katika makazi ya wananchi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.