LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA “waalimu waandaliwa kuelekea Juni 29”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Shirika la kuwajengea uwezo kiuchumi wanawake na wasichana (Mikono Yetu) kwa kushirikiana na Shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana (KIVULINI) limeandaa mafunzo kwa waalimu wa masomo ya Sayansi katika Manispaa ya Ilemela ili kuwajengea uwezo wa kuchukua tahadhari dhidi ya Corona Shule zitakapofunguliwa Juni 29, 2020.

Baada ya waalimu hao kupata mafunzo hayo ikiwemo pia utengenezaji wa sababuni za kunawia mikono, watafikisha elimu hiyo kwa waalimu wenzao pamoja na wanafunzi na hivyo kuamsha ari ya masomo huku tahadhari dhidi ya Corona ikiendelea kuchukuliwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Shirika la Mikono Yetu lilikabidhi mitambo ya kunawia mikono, sabuni pamoja na vipaza sauti katika Shule za Kaselya, Bujingwa pamoja na Buswelu zilizopo Manispaa ya Ilemela.
 Waalimu waliohudhuria mafunzo hayo wakimsikiliza Afisa Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Ilemela, Benatus Kahuru (kulia) wakati akikabidhi vifaa vya kusaidia mapambano dhidi ya Corona pamoja na vidumu kwa ajili ya mafunzo ya kutengeneza sabuni.
 Afisa Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Ilemela, Benatus Kahuru (katikati) akimkabidhi Mwalimu wa Shule ya Msingi Buswelu kipaza sauti kwa ajili ya kusaidia kutoa elimu ya Corona kwa wanafunzi. Kulia ni Mkurugenzi Shirika la Mikono Yetu, Maimuna Kanyamala.
 Waalimu wa Sayansi kutoka Shule za Msingi 30 Manispaa ya Ilemela wakiwa kwenye mafunzo ya namna ya kutengeneza sabuni.
Waalimu wa masomo ya Sayansi kutoka Shule 76 zilizopo Manispaa ya Ilemela watanufaika na mafunzo hayo.
Shirika la KIVULINI litakabidhi matenki 26 yenye ujazo wa lita 1,000 kila moja katika Halmashauri za Misungwi (10), Shinyanga Vijijini (08) na Kishapu (08) ili kusaidia unawaji katika Shule mbalimbali.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.