LIVE STREAM ADS

Header Ads

Sheria ya Miradhi kufanyiwa marekebisho

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
WiLDAF Tanzania – Envisions The Society That Observe Women's Human ...
Na Ramashan Juma
Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika (WilDAF) limesema kuwa Serikali inaendelea kufanyia marekebisho ya sheria mirathi ili kuweza kutoa haki kwa wajane pindi wanapokuwa wamefungua shauri linalohusiana na mirathi.

Akizungumzia kilele cha siku wajane duniani 2020, Mwanasheria wa Shirika hilo Zakia Msangi alisema kuwa serikali imekuwa karibu katika kuhakikisha maboresho ya sheria ya mirathi kwa wajane inaboreshwa na kazi hiyo wameendelea kuifanya kuweza kupata maboresho hayo.

Alisema kumekuwa na majadiliano ya wadau mbalimbali wanaoangazia masuala ya sheria ya wajane na watoto ambapo Serikali imekuwa ikishiriki kwa kuchukua mawazo katika kuweza kufanya maboresho ya sheria hizo.

"Tumeona dhamira ya serikali katika kufanyia marekebisho sheria ya mirathi hii itatoa haki kwa wajane ambapo ni tofauti na ilivyo kwa sasa kwani wajane wengi hawajui hata namna ya kuweza kufungua shauri la mirathi katika mahakama" alisema Msangi.

Aliongeza katika maboresho juu kuwepo kwa adhabu ya wafujaji mali za marehmu ili kuweza kuwa fundisho kwa wengine wanaokimbilia mali huku wakiacha wajane wakiteseka.

Nae Mkurugenzi wa Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) Rose Sarwatt alisema katika maadhimisho hayo kufanya ni mara sita na kuwa na mwitikio mkubwa wanawake wajane katika kufikisha kilio chao katika masuala yanayowazunguka.

Alisema kuwa wana ofisi katika kila kanda ambapo wajane wengi wamekuwa na changamoto katika mirathi kutokana na mila na desturi ya wanawake kutopewa kipaombele pindi anapoondokewa na mwenza wake.

Mjane Faith Mwansye-Okoyo alisema wajane wanapitia katika changamoto kubwa pindi ndugu wa marehemu wanapofika katika kuhakikisha wanamiliki mali bila kujua hata mahitaji ya watoto.

Alisema kuwa katika suala muhimu ni kuwa na Utamaduni wa kuandika wosia kwa pande zote hali ambayo itapunguza dhuruma za mali za marehemu.

No comments:

Powered by Blogger.