LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waliochangia ujenzi wa wodi ya Saratani Bugando watunukiwa vyeti

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Mkuu wa Idara ya Saratani katika Hospitali ya Kanda Bugando iliyopo jijini Mwanza, Dkt. Nestory Masalu (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusiana na huduma za Saratani zinazotolewa na hospitali hiyo kwa baadhi ya wadau waliochangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wodi ya wagonjwa wa Saratani.

Katika kufanikisha ujenzi wa jengo hilo litakalogharibu shilingi bilioni nne, Hospitali ya Bugando imewahimiza wadau mbalimbali kuendelea kuchangia upatikanaji wa fedha hizo ambapo imetenga shilingi Bilioni moja, wafanyakazi wamechangia milioni 250 huku wadau wakichangia milioni 50 hivyo pungufu ikiwa ni shilingi bilioni 2.7.

Uongozi wa Hospitali ya Bugando Juni 24, 2020 umewakabidhi vyeti vya shukurani wadau ambao tayari wamewasilisha michango yao kwa ajili ya ujenzi wa wodi hiyo. 
Michango inapokelewa kupitia benki ya CRDB akaunti namba 01J105452400 jina BMC ama LIPA KWA M-PESA kupitia namba 5500297 jina BMC.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Idara ya Saratani katika Hospitali ya Kanda Bugando, Dkt. Nestory Masalu (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa wadau hao namna tiba ya mionzi inavyofanyika kwa wagonjwa wa Saratani.
 Ujenzi wa wodi ya wagonjwa wa Saratani utaondoa adha kwa wagonjwa kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambao wamekuwa wakipata matibabu katika Hospitali ya Bugando.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.