LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakusanya ushuru Ukerewe wasakwa “warejeshe Milioni 274”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameagiza kukamatwa kwa wakusanya ushuru watano katika Halmashauri ya Wilaya Ukerewe wanaotuhumiwa kuhusika na upotevu wa shilingi milioni 274.6 pamoja na mashine tano za kukusanyia ushuru (POS).

Mongella ametoa agizo hilo kwa Mkuu wa Polisi Wilaya Ukerewe pamoja na Mkuu wa TAKUKURU wilayani humo kuwakamata watuhumiwa hao ambao ni Leopard Musiba, Fortunatus Mutesigwa, Thomas Bagetilanya, Frola Ntale na Didas Majura ili ndani ya wiki moja wawe wamerejesha fedha hizo.

Mongella alitoa agizo hilo Juni 04, 2020 wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Ukerewe cha kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/19.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.