LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya CRDB yazindua huduma ya “QR CODE” jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Benki ya CRDB imezindua huduma ya kukusanya maoni kwa wateja wake kupitia mfumo wa kidijitali (QR Code) katika Jiji la Mwanza hatua itakayowarahisishia wateja kutoa maoni na kuhudumiwa kwa wakati.

Uzinduzi wa huduma hiyo ulifanyika Jumatatu Julai 13, 2020 katika benki ya CRDB tawi la Mwanza ikiwa ni utekelezaji kwa vitendo kauli mbiu isemayo “TUNAKUSIKILIZA” ambapo kwa mara ya kwanza nchini huduma hiyo ilizinduliwa mwezi Machi mwaka huu jijini Dar es salaam.

Awali kulikuwa na mzunguko mrefu kwa wateja kutoa maoni kupitia matawi ya CRDB tofauti na mfumo huo mpya ambao popote mteja alipo anaweza kutumia simu janja yake na kuhudumiwa.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.