LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ilani ya CCM yatekelezwa vyema wilayani Bunda

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Mkuu wa Wilaya Bunda mkoani Mara, Mwl. Lyidia Bupilipili amesema Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/20  imetekelezwa vyema katika Wilaya hiyo katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, umeme na uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mikopo ya Halmashauri.

Mwl. Bupilipili aliyasema hayo Juni 30, 2020 wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani hiyo na kubainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli miradi mipya na ukarabati wa miradi ya zamani imefanyika kwa mafanikio makubwa.

Hata hivyo licha ya mafanikio hayo, Mwl. Bupilipili alisema changamoto ilikuwa upande wa matukio ya ukatili wa kijinsia na hivyo kutumia fursa hiyo kuwaomba viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini kusaidia kupambana na matukio hayo ikiwemo vipigo kwa wanawake pamoja na utoroshaji wanafunzi wa kike kwani vitendo hivyo vinakwamisha juhudi za maendeleo.
#BMG Habari 
 Mkuu wa Wilaya Bunda mkoani Mara, Lyidia Bupilipili akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/20.
 Wananchi na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Bunda, Lyidia Bupilipili wakati akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/20.
 Wananchi na viongozi mbalimbali Wilaya Bunda wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/20 iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Lyidia Bupilipili.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.