LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mzee Mkapa azikwa Masasi mkoani Mtwara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo kwenye kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William Mkapa katika mazishi yaliyofanyika Kijiji cha Lupaso Wilaya Masasi mkoani Mtwara, Jumatano Julai 29, 2020.
Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akishuhudia Mama Anna Mkapa ambaye ni Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa (katikati) akiweka udongo kwenye kaburi.
Wanajeshi wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kuelekea eneo la makaburi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya mazishi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa yaliyofanyika Kijiji cha Lupaso wilayani Masasi.
Mabregedia Jenerali wa JWTZ wakishuhudia Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa likishushwa kaburini. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiwa pamoja na Mama Anna Mkapa ambaye ni Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa wakati wakielekea kuweka udongo kwenye kaburi. Mzee Mkapa alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 24, 2020 jijini Dar es salaam kwa ugonjwa wa moyo.
Picha na IKULU

No comments:

Powered by Blogger.