LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mansoor aungana na watanzania kumuaga Mzee Mkapa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya MOIL, Altaf Hiran Mansoor (pichani juu) ameungana na watanzania pamoja na viongozi mbalimbali ndani na nje ya nchi kuomboleza kifo cha Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mzee Benjamin William Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 24, 2020.

Jumapili Julai 26, 2020 Mansoor alifika nyumbani kwa Mzee Mkapa Masaki jijini Dar es salaam kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Mzee Mkapa na pia kusaini kitabu cha maombolezo.
Shughuli ya siku tatu ya kuuaga mwili wa Mzee Mkapa imehitimishwa kitaifa Jumanne Julai 28, 2020 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo viongozi mbalimbali ndani na nje ya nchi wakiongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wamehudhuria kabla ya mwili huo kusafirishwa kwa ndege kuelekea Masasi mkoani Mtwara kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumatano Julai 28, 2020.
 Viongozi mbalimbali akiwemo Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya MOIL, Altaf Hiran Mansoor wakiwa kwenye shughuli ya kuuaga mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Mkapa aliyefariki Julai 24, 2020 akiwa na umri wa miaka 82 (alizaliwa mwaka 1938 Masasi mkoani Mtwara).
 Umati wa wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla ya kitaifa ya kuuagwa mwili wa Hayati Mzee William Mkapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Msafara wa gari maalum ya JWTZ ikiwa imeubeba Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa.
#BMGHabari

No comments:

Powered by Blogger.