LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakazi wa Misungwi wanufaika na kadi za Bima ya afya bure

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda amekabidhi kadi za bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) katika Kaya mbalimbali wilayani humo kupitia mradi wa PAMVERC ili kuwasaidia kuondokana na adha ya matibabu.

Kupitia mradi huo ulioanza mwaka 2018 na kufikia tamati mwaka 2022, wananchi wamekabidhiwa bure vyandarua pamoja na kadi za bima ya afya ikiwa ni sehemu ya afua za kupambana na Malaria.

Mradi wa PAMVERC unalenga kupambana na ugonjwa wa Malaria kupitia tafiti mbalimbali zinazofanyika katika Kata 17 wilayani Misungwi zenye Kaya 6,300 sawa na wanufaika 37,000.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akizungumza na wananchi katika Kata ya Ukiriguru kabla ya kukabidhi kadi za bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) kupitia mradi wa PAMVERC.
 Meneja mradi wa PAMVERC wilayani Misungwi, Eliud Lukole akielezea utekelezaji wa mradi huo unaolenga kupambana na Malaria kupitia tafiti mbalimbali ikiwemo njia sahihi za kujikinga na ugonjwa huo.
 Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akimkabidhi kadi ya bima ya afya mmoja wa wakazi wa Kata ya Ukiriguru kupitia mradi wa PAMVERC. 
Mmoja wa wakazi wa Ukiriguru (kushoto) akipokea kadi ya bima ya afya kutoka kwa  Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda. 
 Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda (kulia) akimkabidhi mmoja wa wakazi wa Kata ya Ukiriguru kadi ya bima ya afya iliyoboreshwa.
Mgeni rami Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaya mbalimbali wilayani humo zilizokabidhiwa kadi za bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF).
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.