LIVE STREAM ADS

Header Ads

Klabu ya Wanahabari Mwanza yazindua Blogu yake

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) imezindua Blog yake rasmi leo Julai 20, 2020 kwa ajili ya kuhamasisha habari za mkani Mwanza.

Hafla ya uzinduzi wa blogu hiyo ilijumuisha wanachama wa MPC na vyombo mbalimbali vya habari.

Mgeni rasmi Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mkuu Kanda wa TCRA aliipongeza MPC kwa hatua hiyo muhimu ya kuwa na blogu yake.

Pia Mihayo aliongoza zoezi la kukata utepe na kushuhudia muonekano wa blogu hiyo.

Mwenyekiti wa MPC bwana Edwin Soko alisema blogu hiyo ni fursa kwa klabu na wanachama wa MPC.

Soko aliwahimiza waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa kufuata misingi ya taaluma ya habari kuelekea uchaguzi mkuu.

Naye Mkurugenzi wa UTPC Bwana Abubakar Karsan aliipongeza MPC kwa kufanikiwa kuwa na blogu na kuitaka waanzishe bodi ya uhariri mapema ili ianze kufanya kazi kwa weledi.

Pia Karsan aliwataka waandishi wa habari kuripoti habari zao kwa weledi mkubwa hasa kwenye kuelekea uchaguzi mkuu.

No comments:

Powered by Blogger.