LIVE STREAM ADS

Header Ads

Katibu Mkuu Wizara ya Afya avutiwa na Kituo cha Watoto Soko la Kiloleli Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu amevutiwa na ujenzi wa Kituo cha Kupumzikia Watoto katika Soko la Kiloleli lililopo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza na kuhimiza masoko mengine nchini kuwa na vituo vya aina hiyo.

Dkt. Jingu ameyasema hayo Agosti 24, 2020 alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa soko la kisasa Kiloleli unaojumuisha uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo Vyoo, Kituo cha Daladala pamoja na Kituo cha Watoto Kupumzikia/ na akina mama kunyonyeshea.

"Nitakuwa Balozi wenu, kokote nitakakopita nitawaambia waige mfano huu. Hili ni jambo kubwa, hongereni sana" ameeleza Dkt. Jingu huku akifurahishwa pia na mpango wa wafanyabiashara wa Soko la Kiloleli kuchangia gharama kwa ajili ya walezi wa watoto watakaokuwa kwenye Kituo hicho.

Ujenzi wa soko la kisasa Kiloleli pamoja na uboreshaji wa miundombinu yake unatokana na juhudi za shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake (KIVULINI) lililosaidia upatikanaji wa gharama za ujenzi huo kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 lengo likiwa ni kuondoa changamoto kwa wafanyabiashara wadogo hususani akina mama.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Kiloleli.
Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya akiwapongeza wafanyabiashara wa soko la Kiloleli.
Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akifuatilia jambo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu.
Mmoja wa akina mama wafanyabiashara wa soko la Kiloleli amesema manufaa ya ujenzi wa Kituo cha Kupumzikia Watoto sokoni hapo ni pamoja na kuchochea malezi na makuzi bora kwa watoto.

No comments:

Powered by Blogger.