LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi kuanza kunufaika na madini ya bati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko Julai 09, 2020 amefanya ziara katika machimbo ya bati (TIN) katika Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera na kueleza kuwa madini hayo yataanza kusafirishwa nje ya nchi baada ya kuongezewa thamani. Serikali ilizuia madini ghafi ya bati kusafirishwa nje ya nchi baada ya kuona hakuna tija kwa wachimbaji pamoja na Taifa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali pia alitembelea kiwanda cha kuchakata madini ya chuma cha Tanzaplus Minerals na kueleza kuwa Serikali kupitia Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) kununua madini hayo ili kukuza zaidi soko la wachimbaji wadogo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko pia alitembelea ujenzi wa kiwanda cha kuchakata madini ya bati cha ATM (African Tin Minerals).
Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi wa kiwanda cha ATM (kushoto) alipotembelea ujenzi wa kiwanda hicho.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya bati pamoja na wafanyabiashara wa madini hayo wilayani Kyerwa.
Mkuu wa Wilaya Kyerwa, Rashid Mwaimu aliwataka wachimbaji wadogo wa madini ya bati kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia changamoto zao ili kuhakikisha wanafanya shughuli zao kwa tija.
Nao wachimbaji wa madini ya bati walieleza kukabiliwa na changamoto ya soko la uhakika pamoja na bei duni ya madini hayo na kueleza kuwa hatua ya STAMICO kununua madini hayo itaongeza fursa zaidi ya soko.
Wachimbaji wadogo wa madini ya bati wilayani Kyerwa wakimsikiliza Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayuko pichani).
Wachimbaji wadogo wa madini ya bati (TIN) wakifuatilia kikao hicho baina yao na Waziri wa Madini, Doto Biteko.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.