MWANZA “Serikali yasitisha mkataba na mkandarasi wa umeme vijijini”
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Serikali
kupitia Wakala wa Usambazaji Umeme Vijini (REA) imevunja mkataba na Mkandarasi
kampuni ya NIPO Group iliyokuwa ikisambaza umeme katika Vijiji mbalimbali
mkoani Mwanza.
Maamuzi hayo
yameridhiwa kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa REA kilichoketi Jumatatu
Agosti 03, 2020 jijini Mwanza baada ya kuelezwa kuwa Mkandarasi huyo ameshindwa
kutekeleza vyema na kwa wakati majukumu yake.
Kufuatua hatua hiyo, kampuni ETDCO ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) imepewa majukumu hayo ya kusambaza umeme katika Vijiji 70 mkoani Mwanza ambavyo havikufikiwa na kampuni ya NIPO Group kupitia mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza ambao utekelezaji wake unaendelea.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
SOMA>>> Habari mbalimbali
No comments: