LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri wa Nishati akagua miundombinu ya Umeme Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amekagua shughuli ya usimikaji miundombinu ya umeme katika Wilaya za Kwimba na Misungwi mkoani Mwanza, inayofanywa na kampuni ya ETDCO ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO).

Mgalu amefanya ukaguzi huyo Agosti 15, 2020 baada ya kampuni ya ETDCO kukabidhiwa kazi ya kusambaza umeme katika Vijiji 70 mkoani Mwanza ambavyo havikufikishiwa huduma hiyo na kampuni ya NIPO Group ambayo mkataba wake umesitishwa kutokana na kusuasua kwa kazi.

Akizungumza katika maeneo mbalimbali aliyokagua miundombinu na kuwasha umeme ikiwemo Zahanati ya Ilula na Shule ya Sekondari Imalilo wilayani Kwimba, Mgalu alisema hadi kufikia mwezi Juni mwaka 2021 Vijiji vyote nchini vitakuwa vimefikishiwa nishati ya umeme.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akiwahimiza wakazi wa Kwimba kutumia kifaa cha UMETA kuunganishiwa nishati ya umeme katika nyumba ndogo ambazo hazihitaji kufanyiwa 'wiring'.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akiongea na wakazi wa Kwimba na kuwaonyesha kifaa cha UMETA ambacho ni maalum kwa ajili ya wananchi kuunganishiwa nishati ya umeme bila kufanya 'wiring'.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa umeme katika Zahanati ya Ilula wilayani Kwimba.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na TANESCO baada ya kuwasili wilayani Kwimba.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Imalilo wilayani Misungwi baada ya kuwasha umeme katika Shule hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akizungumza na viongozi mbalimbali wilayani Misungwi baada ya kukagua maendeleo ya usimikaji miundombinu ya umeme wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza unaotekelezwa na kampuni tanzu ya TANESCO iitwayo ETDCO baada ya kampuni ya NIPO Group kusitishiwa mkataba wake.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.