LIVE STREAM ADS

Header Ads

Afisa wa TRA anaswa na TAKUKURU kwa tuhuma za RUSHWA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Mwanza imemkamata Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mary Moyo (34) kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara mmoja jijini Mwanza.

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa Mwanza, Daudi Ndyamukama (pichani juu) amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Septemba 26, 2020 baada ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni nane kutoka kwa mfanyabiashara huyo (jina limehifadhiwa) ili amrekebishie hesabu alizokuwa anadaiwa TRA kutoka shilingi milioni 97,156,994 hadi kufikia milioni 35,000,000 ambapo angelipa milioni 27,000,000 kwa 'control number' na milioni nane angechukua afisa huyo wa TRA.
#BMGHabari
Wanahabari wakimsikiliza Afisa Mahusiano wa TAKUKURU mkoani Mwanza.
Maafisa wa TAKUKURU.
Wanahabari
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.