LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanahabari watakiwa kuchangamkia fursa NHIF

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango wa huduma ya Bima ya Afya ya NHIF kwa Waandishi wa Habari. Uzinduzi huo wa kitaifa umefanyika Septemba 14, 2020 jijini Mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewahimiza waandishi wa habari nchini kujiunga kwa wingi na mfuko huo ili kunufaika na huduma ya matibabu baada ya kujumuishwa kwenye mpango wa kunufaika na bima ya afya NHIF.

Mkurugenzi Mkuu wa NHFI, Benard Konga aliyasema Septemba 14, 2020 jijini Mwanza wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango wa Bima ya Afya kwa kundi la waandishi wa habari.

Naye Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo aliwataka waandishi wa habari kuonyesha mwitikio mkubwa wa kujiunga na bima ya afya ya NHIF huku wakitumia vyema wajibu wao kuelimisha wananchi kujiunga na huduma hiyo.

Awali Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPIC), Deogratius Nsokolo alieleza kutoridhishwa na mwitikio mdogo wa waandishi wa habari ambao tayari wamejiunga na bima ya afya ya NHIF akisema kati ya 1800 waliojiunga ni 65 na wategemezi wao 20.

Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa Mwanza (MPC) kupitia kwa Mwenyekiti wake Edwin Soko ilitoa wazo la waandishi wa habari nchini kujumuishwa kwenye mpango wa bima ya afya kwenye mkutano wa wadau wa NHIF uliofanyika Disemba 2019 jijini Mwanza.

Ili kunufaika na bima hiyo, mwandishi atapaswa kulipia shilingi laki moja na shilingi themanini ambapo sharti kubwa ni lazima awe mwanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari katika Mkoa husika hapa nchini.Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza, Edwin Soko.Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan (kulia) akipokea kadi ya NHIF kwenye uzinduzi wa mpango wa Bima ya Afya kwa Waandishi wa Habari.Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.Wanahabari.Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Benard Konga (kulia) pamoja na Meneja wa NHIF (kushoto) wakifuatilia hafla hiyo.Rais wa UTPC, Deogratius Nsokolo.Wanahabari na wadau wakifuatilia hafla hiyo.Mkurugenzi Mkuu NHIF, Benard Konga.Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

SOMA>>> Matukio mbalimbali ya Wanahabari

No comments:

Powered by Blogger.