LIVE STREAM ADS

Header Ads

"Chagueni CCM mpate maendeleo" Mgombea Ilemela

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wananchi wakimsikiliza mgombea ubunge katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza kupitia CCM, Dkt. Angeline Mabula.
Na Tonny Alphonce, Ilemela
Wananchi wa Kata ya Buzuruga jimboni Ilemela wameadiwa kujengewa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi ya walimu endapo watachagua viongozi wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya urais, ubunge na udiwani.

Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Dkt Angeline Mabula ametoa ahadi hiyo kwenye mkutano wake wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Nyambiti.

Alisema shilingi milioni 146.5 zimetengwa kwa ajili ya kujenga vyumba hivyo vya madarasa ambapo viwili ni katika shule ya Msingi Nyambiti na chumba kimoja ni katika Shule ya Msingi Amani. Aliongeza kuwa ujenzi wa ofisi ya waalimu utakuwa katika Shule ya Msingi Nyambiti. 
Mgombea ubunge jimbo la Ilemela kupitia CCM, Dkt. Angeline Mabula.

Aidha Dkt. Angeline alibainisha kuwa lengo la Serikali ni kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia na kuhakikisha Wilaya ya Ilemela inaendelea kushika nafasi ya juu katika matokeo ya kitaifa.

Kwa upande wa sekta ya afya, Dkt Angeline alisema kituo cha afya Buzuruga kilitengewa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu mbalimbali ambapo fedha hizo zilitumika kujenga majengo ya maabara, jengo la kuhifadhi maiti, jengo la kufulia, jiko na jengo la kufanyia upasuaji ambalo limekamilika na hivi karibuni litaanza kutumika.
Mgombea ubunge jimbo la Ilemela kupitia CCM, Dkt. Angeline Mabula (kulia) akimnadi mgombea udiwani Kata ya Nyambiti (kushoto).

No comments:

Powered by Blogger.