LIVE STREAM ADS

Header Ads

ILEMELA "Mabula awataka wananchi kutofanya makosa tena"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Tonny Alphonce, Ilemela
Mgombea ubunge katika jimbo la Ilemela kupitia CCM, Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi wa Kata ya Nyamanoro jimboni humo kumchagua mgombea udiwani wa CCM ili aweze kushirikina nae katika kuwaletea maendeleo.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wake wa kampeni Dkt. Mabula alisema Kata ya Nyamanoro imekuwa nyuma kimaendeleo kutokana na wana Nyamanoro wenyewe kumchagua diwani wa upinzani ambaye muda wote alikuwa na migogoro ya kisiasa  na wenzake na kushindwa kutatua kero za wananchi kwa wakati.

"Ndugu zangu mkicheza mpira katika timu lazima muwe na mfumo mmoja wa mchezo, hamuwezi mkacheza mfumo wa kushambulia na wengine mfumo wa kurudi nyuma halafu mtegemee kushinda,  haiwezekani na ndio maana nawaomba mniletee Maganiko (mgombea udiwani Kata ya Nyamanoro)" alisisitiza Dkt. Mabula.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela, Nelson Mesha alisema inasikitisha kuona Kata ya Nyamanoro hadi leo haina Shule ya Sekondari, Zahanati na hata Kituo Cha Afya wakati Kata zingine zinajipanga kuongeza Sekondari zaidi hadi kufikia nne.

Mesha aliwataka wana Nyamanoro mwaka huu wahakikishe wanamchagua Dkt. John Pombe Magufuli upande wa urais, Dkt. Angeline Mabula upande wa ubunge na Ngaka Maganiko kwa upande wa udiwani katika Kata ya Nyamanoro.

Kwa miaka kumi Kata ya Nyamanoro ilikuwa ikiongozwa na diwani wa upinzani ambaye kwa miaka yote ya uongozi wake alikuwa akikumbana na migogoro ya kisiasa ambapo mwaka 2014 alivuliwa nafasi ya udiwani na aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata na mwaka 2015 ushindi wake ulipingwa mahakamani na aliyekuwa mgombea wa CCM, Ngaka Maganiko.

SOMA>>> Habari kutoka Ilemela

No comments:

Powered by Blogger.