LIVE STREAM ADS

Header Ads

Sengerema Seminari yaadhimisha Jubilee ya Miaka 25

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shule ya Sengerema Seminari iliyopo Wilaya Sengerema mkoani Mwanza imeadhimisha Jubilee ya Fedha (miaka 25) tangu kuanzishwa kwake mwaka 1995 huku msisitizo mkubwa ukitolewa kwa wazazi kuwalea watoto katika misingi ya maadili.

Maadhimisho hayo yalifanyika Jumamosi Oktoba 03, 2020 katika viunga vya shule hiyo iliyo chini ya Kanisa la Romani Katoliki (RC) Jimbo la Geita ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.

Pia maadhimisho hayo yaliambatana na mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne Sengerema Seminari pamoja na harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa katika Seminari hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Sengerema Seminari.
Askofu wa Kanisa la Romani Katoliki (RC) Jimbo la Geita, Flavian Kasalla akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.
Mkuu wa Shule ya Sengerema Seminari, Padri Francis Muganyizi akisoma risala ya miaka 25 tangu kuanzishwa shule hiyo.
Askofu wa Kanisa la Romani Katoliki (RC) Jimbo la Geita, Flavian Kasalla (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) zawadi ya vikombe maalum vya Jubilee ya miaka 25 tangu kuanzishwa Shule ya Sengerema Seminari mwaka 1995.
Wahitimu wa kidato cha nne Sengerema Seminari mwaka huu 2020 wakiwa kwenye maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya shule hiyo yaliyoambatana na mahafali ya wahitimu hao.
Waalikwa mbalimbali.
Waalikwa mbalimbali wakishiriki harambee ya ujenzi wa kanisa katika Shule ya Sengerema Seminari.
Ujenzi wa kanisa katika shule ya Sengerema Seminari umefikia hatua ya upauaji ambapo kwenye maadhimisho hayo ilifanyika harambee kukusanya fedha za kukamilisha ujenzi huo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.