TANESCO Mwanza waadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Akizungumza kwenye hafla fupi iliyowajumuisha wafanyakazi pamoja na wateja, Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Henryfried Byabato ameahidi kuwa shirika hilo litaendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuwaunganishia nishati ya umeme wateja wapya ndani ya siku 14 baada ya kufanya malipo.
Nao baadhi ya wateja waliojumuika kwenye hafla hiyo wakakiri TANESCO kuboresha huduma zake huku wakitoa rai kwa shirika hilo kutoa taarifa kwa wakati pindi kunapokuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
No comments: