RC MONGELLA azindua matawi ya benki ya NCBA jijini Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amezindua rasmi matawi mawili ya benki ya NCBA yaliyopo barabara za Nyerere na Kenyatta jijini Mwanza na kuhimiza benki hiyo kuwa kichochea cha ukuaji wa uchumi wa wananchi.
RC Mongella amefanya uzinduzi huo Ijumaa Oktoba 02, 2020 katika tawi la benki hiyo lililopo barabara ya Kenyatta akisema kuwa anategemea kuona benki ya NCBA ikija na huduma zitakazosaidia wafanyabiashara hususani wadogo mkoani Mwanza kujiimarisha kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo viwanda, uvuvi na kilimo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NCBA, Margareth Karume amesema ujio wa benki hiyo ni majibu sahihi ya huduma bora za kifedha kwa wananchi ambapo shabaha kubwa ni kurahisisha upatikanaji wa fedha ikiwemo mikopo kwa wateja wake ili kukuza biashara ndogo, za kati na kubwa.
Ujio wa benki ya NCBA unatokana na muunganiko wa benki mbili ambazo ni NIC pamoja na CBA uliofanyika Julai 08, 2020 na tayari imezindua matawi yake Dar es salaam, Arusha na Zanzibar huku pia ikiwa na matawi mbalimbali barani Afrika.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa tatu) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa matawi ya benki ya NCBA jijini Mwanza. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Emmanuel Tutuba (wa pili kulia), Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Muliro Jumanne (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NCBA, Margareth Karume (wa pili kushoto).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akizungumza kwenye uzinduzi huo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji benki ya NCBA, Margareth Karume.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati), Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Emmanuel Tutuba (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji NCBA, Margareth Karume (kushoto).
Uzinduzi huo uliambatana na shamrashamra katika mitaa mbalimbali jijini Mwanza.
Wafanyakazi mbalimbali wa benki ya NCBA wakiwa kwenye shamrashamra za uzinduzi wa matawi ya benko hiyo jijini Mwanza.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
SOMA>>> Habari mbalimbali za kibenki
No comments: