LIVE STREAM ADS

Header Ads

BIBI WA MIAKA 90 APATA HAKI YAKE BAADA YA KUHANGAIKA MUDA MREFU

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Bibi Annastazia Ndazi anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 90 amepata haki yake baada ya Baraza la Ardhi Wilaya Mwanza kumrejeshea ardhi yake yenye upana wa mita 30 na urefu wa mita 60 katika eneo la Bwiru Ziwani katika Manispaa ya Ilemela.

Tangu mwaka 2012 bibi huyo alikuwa akihangaika kusaka haki hiyo baada ya Mzee Yohana Magayane kuipokonya kwa nguvu na kisha kumfungulia mashitaka mahakamani ili kuwa na uhalali wa kumiliki eneo hilo. 

Akitoa uamuzi huo Novemba 13, 2020 katika kesi namba 179 ya mwaka 2012, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mayeye Magambo alimtaka mzee Magayane kuondoka katika eneo hilo mara moja na kisha kumjengea bibi huyo nyumba ya vyumba vitatu aliyoibomoa. 

Baada ya kupata haki yake hiyo, bibi Ndazi aliishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na wadau mbalimbali ikiwemo shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake (KIVULINI) kwa kuhakikisha hadhurumiwi ardhi yake ikizingatiwa hana mtoto huku mlalamikaji mzee Magayane akieleza kutoridhika na hukumu hiyo.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.