LIVE STREAM ADS

Header Ads

Asasi ya "Teach For Tanzania" yasaida kuboresha Sekta ya Elimu Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Asasi ya Teach For Tanzania imetoa mafunzo kwa waalimu viongozi 36 awamu ya pili katika kambi ya wiki sita iliyiofanyika katika Wilaya Magu mkoani Mwanza ambapo lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo kutimiza vyema majukumu yao ya ufundishaji na uongozi. 

Akizungumza kwenye kilele cha mafunzo hayo Novemba 13, 2020, Mkurugenzi wa asasi hiyo Sophia Assenga alisema wahitimu hao watasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii hususani kusaidia maendeleo ya elimu katika Shule watakazopangiwa. 

Assenga alisema kuanzia mwakani 2021 wahitimu hao watakuwa na jukumu la kufundisha katika Shule za Msingi na Sekondari kwa kipindi cha miaka miwili huku akibainisha kuwa awamu ya kwanza ya mafunzo ya aina hiyo yalitolewa kwa waalimu viongozi 28 ambao wamepangiwa kufundisha katika Shule 12 za Wilaya za Bunda na Serengeti mkoani Mara. 

Nao wahitimu wa mafunzo hayo awamu ya pili walisema yamewajengea mbinu mbalimbali ikiwemo za ufundishaji na ujifunzaji na hivyo kutekeleza kwa weledi majukumu yao kwa lengo la kuboresha maendeleo ya elimu Tanzania huku wakiiomba asasi ya Teach For Tanzania kutanua wigo wake zaidi ili kuyafikia maeneo mengi nchini kwani uhitaji ni mkubwa. 

Asasi ya Teach For Tanzania pia imeendesha mafunzo kwa waalimu 725 walio kazini katika Wilaya za Magu, Misungwi, Serengeti na Bunda kupita mradi wa Profuturo Afrika unaotekelezwa pia katika nchi za Liberia na Nigeria ambapo kwa pamoja Teach For Tanzania, Teach For Liberia na Teach For Nigeria wametoa mafunzo kwa waalimu 15,000 walio kazini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa taasisi ya Teach For Tanzania, Sophia Assenga akizungumza kwenye kilele cha mafunzo kwa waalimu viongozi yaliyofanyika katika Wilaya Magu mkoani Mwanza yakiwajumuisha washiriki 36.
Afisa Elimu Maalum Wilaya Magu, Mwl. James Mgabe akitoa salamu zake wakati wa kilele cha mafunzo kwa waalimu viongozi yaliyofanyika wilayani humo kwa muda wa wiki sita.
Wadau mbalimbali wakitoa salamu zao kwenye hafla hiyo.
Picha mbalimbali wahitimu pamoja na viongozi wao.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.