LIVE STREAM ADS

Header Ads

Chuo Kikuu CUHAS chaunga mkono jitihada za Serikali

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya, Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za Afya (CUHAS) kwa kushirikiana na Hospitali ya Kanda Bugando kimeendelea kuzalisha wahitimu wenye sifa.

Aidha baadhi ya wahitimu wa chuo hicho tayari wameanza kufanya tafiti kuhusiana na magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani ili kutoa na suluhisho la magonjwa hayo kama Rais Dkt. John Pombe Magufuli alivyoagiza mwaka jana wakati akizindua huduma za tiba katika Hospitali ya Bugando. 

Hayo yamebainishwa na uongozi wa chuo hicho wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwemo mahafali ya 13 yanayotarajiwa kufanyika jumamosi Novemba 14, 2020 katika viunga vya Hospitali ya Bugando.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha CUHAS, Prof. Paschalis Rugarabamu (kulia) akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na mahafali ya 13 ya wahitimu wa chuo hicho.
Timu ya wataalamu mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha CUHAS wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Paschalis Rugarabamu (katikati meza kuu).
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.