LIVE STREAM ADS

Header Ads

DKT. JINGU AWATAKA MAAFISA USTAWI WA JAMII KUONGEZA UWAJIBIKAJI

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu amehitimisha kongamano la Wataalamu wa Ustawi wa Jamii lililofanyika jijini Mwanza. 

Dkt. Jingu ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa Chama cha Wataalamu wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) kusimamia miiko ya wataalamu hao ili kuhakikisha wanatimiza vyema majukumu yao. 

Alisema licha ya kazi nzuri inayofanywa na wataalamu wa Ustawi wa Jamii, bado kuna watumishi wachache wakiwemo Maafisa Ustawi wa Jamii ambao hawatimizi vyema wajibu wao na kuwa sehemu ya kusababisha migogoro kutokana na maamuzi yao.

"Nimepata malalamiko baba mmoja analalamika amenyang'anywa mtoto kwa sababu mama amecheza michezo flani na Afisa Ustawi wa Jamii" alionya Dkt. Jingu huku akiongeza kwamba pia kuna Vituo vya Kulelea Watoto havikidhi vigezo lakini taarifa za Maafisa Ustawi wa Jamii zinaonyesha viko sawa jambo ambalo si sawa na Serikali imeanza ukaguzi na haitasita kuvifungia.

Naye Mwenyekiti wa TASWO, Dkt. Mariana Makuu amepongeza ushirikiano unaotolewa na Serikali kwa Wataalamu wa Ustawi wa Jamii wakati wa kushughulikia majanga mbalimbali ikiwemo janga la hivi karibuni la Covid 19 (Corona) ambapo wataalamu hao walishiriki katika hatua zote. 

"Pia tunampongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa namna alivyotuongoza kwenye mapambano dhidi ya Corona, tuliondoa hofu katika jamii na kwa uwezo wa Mungu tukashinda" amesema Makuu. 

Pia Dkt. Makuu aliomba Serikali kusaidia upatikanaji wa Sheria ya Ustawi ambayo itasimamia vyema weledi wa taaluma ya Ustawi wa Jamii.

Kongamano la Wataalamu wa Ustawi wa Jamii liliambatana na Mkutano Mkuu wa TASWO kuanzia Novemba 25-27, 2020 ili kujadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuboresha taaluma ya ustawi wa jamii.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu akizungumza kwenye kilele cha kongamano la wataalamu wa Ustawi wa Jamii lililofanyika jijini Mwanza.
Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii Tanzania wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASWO), Dkt. Mariana Makuu akitoa neno kuhusiana na kongamano hilo.
Wanahabari wakinasa matukio wakati wa kufunga kongamano hilo.
Viongozi mbalimbali meza kuu akiwemo Kamishina wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Naftali Ng'ondi (kulia).
Wataalamu wa Ustawi wa Jamii Tanzania wakiwemo Maafisa Ustawi wa Jamii wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo.
Kongamano la Wataalamu wa Ustawi wa Jamii Tanzania limeambatana na Mkutano Mkuu wa TASWO.
Kongamano na Mkutano Mkuu wa TASWO kwa pamoja
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.