LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella afungua mkutano wa Wataalamu wa Ustawi wa Jamii "awataka kujitambua"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amewataka wataalamu wa ustawi wa jamii kurudisha heshima na nafasi ya taaluma ya ustawi wa jamii kwa kueleza kazi nzuri na kubwa wanayoifanya katika kuwatumikia wananchi. 

Mongella alitoa rai hiyo Jumatano Novemba 25, 2020 wakati akifungua mkutano wa mwaka wa chama cha wataalamu wa ustawi wa jamii Tanzania (TASWO) unaofanyika kwa siku tatu jijini Mwanza. 

Alisema wataalamu wa ustawi wa jamii wana nafasi nyeti katika jamii hivyo hawapaswi kujifungia na badala yake wanapaswa kutimiza wajibu wao wa kuisaidia jamii kusonga mbele kimaendeleo hatua ambao pia itafanya watu kutambua umuhimu wa taaluma hiyo. 

“Twendeni tukajihalalishe, watu wakaone umuhimu wetu, turudishe heshima na nafasi ya ustawi wa jamii, na watu watutambue kwamba tupo na tuna nafasi nyeti katika kuisaidia jamii kwenda mbele” alisisitiza Mongella ambaye pia ni mmoja wa wataalamu wa ustawi wa jamii hapa nchini. 

Naye Makamu Mwenyekiti wa TASWO, Awadh Mohamed ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo alisema lengo ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu wa ustawi wa jamii, maafisa wa ustawi wa jamii, Serikali pamoja na taasisi binafsi ili kujadili changamoto, fursa na mipango katika kuwahudumia wananchi. 

“Ni awamu sasa ya kwenda kwenye jamii na ngazi ya taifa kueleza na kuutangaza umuhimu wa kazi za wataalamu wa ustawi wa jamii” alidokeza Mohamed.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akifungua kongamano la wataalamu wa ustawi wa jamii Tanzania.
Wataalamu wa ustawi wa jamii Tanzania wakimsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Katibu wa TASWO akitoa shukurani kwa wadau mbalimbali wanaoshirikiana na chama hicho katika kutimiza majukumu kwenye jamii.
Tazama picha  mbalimbali kwenye mkutano wa mwaka wa TASWO unaofanyika jijini Mwanza.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.