LIVE STREAM ADS

Header Ads

Katibu Mkuu Wizara ya Madini ahitimisha Mkutano wa Wajiolojia "tutaondoa vishoka"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (kushoto) ametembelea banda la Shirika la Taifa la Petroli (TPDC) katika mkutano wa mwaka wa wajiolojia Tanzania uliofanyika jijini Mwanza na kupongeza jitihada za shirika hilo kuanza kusambaza nishati ya gesi katika maeneo mbalimbali ikiwemo majumbani na viwandani.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila amewaonya Wajiolojia wanaopika taarifa za utafiti ili kuwauzia wawekezaji na badala yake wajikite kwenye tafiti zenye tija katika sekta mbalimbali ikiwemo madini, mafuta na gesi.

Prof. Msanjila ametoa onyo hilo Novemba 28, 2020 jijini Mwanza wakati akifunga mkutano wa mwaka wa chama cha wataalamu wa jiolojia Tanzania (TGS).

Amesema ili kupambana na kadhia hiyo, Serikali inaandaa bodi ya usajili wajiolojia ili kuondoa vishoka katika taaluma hiyo huku akitoa rai kwa wajiolojia nchini kutokalia tafiti zao kwenye makabrasha bali wazihuishe kwa vitendo filidi ili kuleta tija kwa taifa.

Hata hivyo Prof. Msanjila amewapongeza wajiolojia wanaotimiza vyema wajibu wao na hivyo kuibua mabilionea wapya katika sekta ya madini pamoja na kuongeza makusanyo katika sekta hiyo.

Awali Rais wa Chama cha Wajiolojia Tanzania (TGS), Pro. Abdulkarim Mruma aliomba kuundwa Bodi ya Usalijili Wajiolojia ili kusaidia upatikanaji wa wataalamu wenye sifa ombi ambalo limekubaliwa na Prof. Msanjila.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (kushoto) pia alitembelea banda la chama cha wajiolojia Tanzania (TGS) kuona shughuli zinazotekelezwa na chama hicho.
Tazama picha mbalimbali...
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.