LIVE STREAM ADS

Header Ads

Daraja la Kigongo-Busisi lapewa jina la JPM "litafahamika kote duniani"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale ametangaza kuwa daraja linalojengwa katika Ziwa Victoria kuunganisha wilaza za Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza (Kigongo-Busisi) sasa litaitwa “daraja la JPM”. 

Mhandisi Mfugale ametangaza mabadiliko ya jina hilo Jumanne Disemba 15, 2020 kwenye hafla fupi iliyohudhuriwa na viongozi pamoja na watendaji mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella. 

“Rais Dkt. John Pombe Magufuli ana historia kubwa katika daraja hili hivyo tumeona ni vyema liitwe jina lake ambapo hii itasaidia kujulikana zaidi pia kote duniani” alisema Mhandisi Mfugale wakati akizungumzia mabadiliko ya jina la daraja hilo ambalo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 600.

Naye Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amepongeza maamuzi ya daraja hilo kuitwa jina la JPM kwani hiyo ndiyo zawadi pekee kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya katika uongozi wake.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) akieleza sababu za kuita daraja linalojengwa eneo la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza jina la "Daraja la JPM". Kulia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Viongozi mbalimbali wakishuhudia hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mtendaji Mkuu TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale pamoja na Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella wakikagua uundaji wa daraja la kupitisha vitaa kwa ajili ya ujenzi wa daraja la JPM eneo la Kigongo-Busisi.
Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale (kulia) akifafanua jambo kuhusiana na ujenzi wa daraja la JPM katika ziwa Victoria eneo la Kigongo-Busisi.
Ukaguzi wa daraja la JPM eneo la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza.
Ujenzi wa daraja la JPM utaondoa adha ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na nchi jirani wanaotegemea kivuko katika eneo la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mtendaji Mkuu TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale na Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mtendaji Mkuu TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale na Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella wakiwa kwenye picha ya pamoja.
"Daraja la JPM hoyeeeeeeee!!!!!"...
Tazama BMG TV hapa

No comments:

Powered by Blogger.