LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanza watakiwa kuchukua tahadhari magonjwa ya mlipuko

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachunzibwa ameeleza kuwa ili jamii iweze kuishi katika mazingira salama na yenye afya ni vema kuchukua tahadhari mapema dhidi ya magonjwa ya mlipuko. 

Dkt. Rutachunzibwa alirleza kuwa katika kipindi hiki cha mvu zinazoendelea kunyesha maeneo mengi nchini ni vema kuchukua tahadhari ili kuhakikisha hakuna magonjwa yanayowapata. 

Mvua hutibua mifumo wa maji taka na wakati mwingine kupelekea kuchanganyikana na mfumo wa maji safi ambayo tunatumia hivyo tahadhari ni muhimu kabla ugonjwa haujatokea na kuwaathiri kwa namna moja ama nyingine. 

Dkt. Rutachunzibwa ameeleza kuwa yapo magonjwa mengi ambayo yanaweza kuibuka katika jamii hususani kwa kipindi hiki cha mvua ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo na ugonjwa wa kipindupindu hivyo ni vema wanachi wakajenga vyoo bora na imara lakini pia kunywa maji yaliyochemshwa.
Tazama BMG TV hapa chini
Na Blandina Aristides, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.